DMM.com ni tovuti iliyoanzishwa kwa kipindi kirefu tangu mwaka 1999, ikitoa mambo mbali mbali (zaidi ya 40) yenye maudhui ya kiburudani. Mtandao huu umekua na kufikia kuwa mtandao mkubwa zaidi nchini Japani, ukifikisha idadi ya watumiaji zaidi ya milioni 19 hadi kufikia mwaka 2015.

Kwa sasa kampuni ya DMM.com imesambaa kote ndani ya nchi na kimataifa, na kuongeza wigo wa huduma zake nje ya teknologia ya mawasiliano huku ikizitazama fursa mpya za kibiashara kwa uharaka na urahisi.

Huduma zetu zipo katika maeneo mbalimbali: SIM (kutoa kadi za SIM kwa simu aina ya smartphone), biashara ya fedha za kigeni, manunuzi kupitia mtandao, michezo kupitia mtandao (online games), huduma ya uchapishaji maumbo (3D Printing), utengenezaji wa maroboti, vipindi vya kujifunza kiingereza, usimamizi wa shughuli na matukio mbalimbali, ##idols promotions##, kukodisha, vioo vya nishati ya jua n.k.

MAJOR SERVICES (HUDUMA ZETU KUU)

ONLINE VIDEO STREAMING DIVISION (KITENGO CHA VIDEO ZA MTANDAONI)

DMM inakuletea maonesho ya moja kwa moja ya kikundi cha AKB48 kupitia mtandao, na kusambaza na kuuza video za kidigitali. Michezo ya kuigiza, filamu, tamthilia , video za michezo, muziki na nyinginezo mbali mbali zinazokaribia kutoka zinapatikana kwa ajili ya kupakuliwa.

Huduma zetu(*Tovuti ya Kijapani)

FX DIVISION (KITENGO CHA BIASHARA YA FEDHA ZA KIGENI)

Kwa kushirikiana na wateja wetu, DMM.com FX ndiyo kampuni ya kwanza nchini Japani, kwa kuwa na akaunti nyingi za watumiaji zilizosajiliwa.
Jozi ya fedha zote 20 zenye viwango vya hali ya juu zinapatikana. Zaidi ya hayo, tunatoa uhakika wa uaminifu kwa kiasi chote na kuweka mazingira salama ya kufanya biashara kwa kuzitenganisha fedha za wateja wetu.
DMM inatoa mfumo rahisi kwa watumiaji wake kufanya biashara kwa urahisi na ufanisi mkubwa, huku ikitoa huduma kwa wateja kwa masaa 24 kwa siku siku zote za kazi ndani ya wiki.

Huduma zetu(*Tovuti ya Kijapani)

ONLINE GAMES DIVISION (KITENGO CHA MICHEZO YA KUJIFURAHISHA MTANDAONI)

DMM iliingia katika soka la michezo ya kujifurahisha mtandaoni (online games) mnamo mwaka 2011. Michezo yetu inapatikana katika vifaa 3: kikubwa ikiwa ni kompyuta (kisakuzi), simu za android (Google Play) na simu za i-phone (i-Store) na kucheza michezo hii yote ni bure kabisa.
Kwa sasa, DMM inaendelea kutanua wigo wa huduma zake kwa kasi nnje ya nchi.

ENGLISH CONVERSATION DIVISION (KITENGO CHA KUONGEA KIINGEREZA)

DMM inaongoza kwa kutoa huduma zinazoridhisha kwa wateja wetu katika soko la kujifunza kiingereza kupitia mtandao. Waalimu wetu wanachaguliwa kwa umakini mkubwa kutoka jumla ya nchi zaidi ya 60 duniani. Unaweza ukapata mafunzo ya kiingereza kwa bei nafuu muda wowote na popote ulipo. Unachohitaji ni kuwa na laptop(kompyuta), tablet au simu tu inayoweza kuwekwa programu ya Skype.
Hautaogopa kuongea kiingereza tena!!

 • E – BOOKS (VITABU VYA KIELEKTRONIKI)

  Unaweza kupakua vitabu mbali mbali maarufu kwenye kompyuta au simu yako kwa ajili ya kujisomea.Hivi vinapatikana masaa 24, na zaidi ya simulizi 10,000 za picha na vitabu 5000 vya picha siku zote vinapatikana katika hifadhi yetu.

 • Online Catalogue Shopping

  DMM inatoa vitu vya aina mbalimbali kama vile DVD, Blue ray, CD , vitabu , michezo ya kujifurahisha (games) n.k. Tuna uhakika kabisa kwamba utapata unachokitafuta! Tunatoa punguzo hadi la asilimia 27 (27%) kwa DVD na Blue ray mpya.

 • SOLAR PANELS (VIOO VYA NISHATI YA JUA)

  DMM ina vioo vyake yenyewe vya nishati ya jua (katika maeneo 16 nchini Japani) na inauza nishati kwa mashirika na makampuni (#utility firms). Kwa kutumia maeneo yanayomilikiwa na makampuni au serikali, kama vile mapaa na ardhi binafsi, DMM inaweza kuweka vioo hivi vya nishati ya jua kadiri mteja atakavyohitaji. Kutumia huduma hii, sio tu kutasaidia kuzalisha umeme bali pia kutunza mazingira.

 • DMM MOBILE (DMM SIMU YA MKONONI)

  Ukiwa unatumia simu aina ya smartphone au tablet, unaweza kutumia huduma ya mtandao (internet) kupiga simu kwa kiwango cha chini cha yen 440 kwa mwezi. DMM inaandaa vifurushi mbalimbali unavyoweza kuchagua kulingana na matumizi yako.

 • DMM.make Robots

  Tunatoa uwanja wa kuuza maroboti, tukiwa ni wafanyabishara tunaoongoza duniani kwa biashara ya maroboti.

 • DMM.yell

  Hii ni application ya kijamii inayounganisha mastaa (wote wavulana na wasichana ) na mashabiki wao.

 • RENT ANYTHING SERVICE (HUDUMA YA KUKODISHA CHOCHOTE)

  Kupitia mtandao wa internet unaweza kukodi zaidi ya vitu 4,100 kama vile mabegi na nguo za kibunifu na vifaa vya kuchezea mchezo wa golfu. Kwa miaka ijayo uelekeo utakua zaidi kwenye kukodi kuiko kununua. Takribani watu 100,000 wametumia huduma hii.

 • DMM LOUNGE (DMM LAUNJI)

  Hii ni huduma ya kuunganisha jamii kwa kutumia akounti zao za facebook. Huduma hii inawaunganisha watumiaji na watu maarufu na mashuhuri kutoka ulimwengu wa biashara, sanaa , michezo n.k

 • OTHER SERVICES (HUDUMA NYINGINEZO)

DMM'S MEMBERSHIP AND SALES (UANACHAMA WA DMM NA MAUZO)

Kuhusu Kampuni

Jina
DMM.com LLC
Anuani
Yebisu Garden Place Tower 21F, 4-20-3 Ebisu, Shibuya-ku, Tokyo 150-6021,JAPAN
Raisi
Takanori Katagiri
Imeanzishwa
17 November 1999
Mtaji
Millioni 30
#mwezi wa fedha
February
Idadi ya waajiriwa
1650 (Jumla kwa #kampuni nzima)

KIKUNDI CHA DMM.com

 • DMM.com

  DMM.com LLC
  System development, Network operation,Infrastructure provision, WEB marketing,Business planning and sales

 • DMM.com Securities

  DMM.com securities Co.Ltd
  Shughuli za biashara ya fedha za kigeni.

 • DMM.com Override

  DMM.com Overide Co.Ltd
  Utengenezaji na Ufanyaji kazi wa michezo ya kujifurahisha, Ubunifu wa 2D /3D ,Ufanyaji kazi wa miundombinu ya michezo ya kujifurahisha.

 • DMM.com Base

  DMM.com Base Co.Ltd
  Ina ujuzi wa mambo ya kisheria na uhasibu kuisaidia kampuni.

 • DMM.futureworks

  DMM.com Futureworks Co.Ltd
  Utengenezaji wa vipindi na video kwa ajili ya ukumbi wa DMM Virtual Reality unaotumia 3DCG Hologram na usimamizi wa ukumbi huo.